![RED_ONE RWANDA_NIGERIA-2241]()
Diamond Platnumz, mwimbaji kiongozi wa kundi la U2, Bono, D’Banj na Banky W wamefanya remix ya wimbo wa Strong Girl, ambao mwanzo ulifanywa na wanamuziki Vanessa Mdee, Arielle T, Blessing, Gabriela, Judith Sephuma, Selmor Mtukudzi, Victoria Kimani, Waje na Yemi Alade.
Katika remix hiyo iliyozinduliwa wiki hii, muigizaji Omotola wa Nigeria ndiye video queen kwenye video kali ya wimbo huo.
Wimbo huo una lengo la kuwaambia viongozi kutilia mkazo uwezejaji na haki za wanawake katika mkutano wa umoja wa mataifa unaoendelea hivi sasa nchini Marekani.
Katika vikao vya wakuu wa nchi kupitisha maelengo dunia ambayo yataweka ajenda za maendeleo kwa kizazi, mastaa hawa wa muziki Afrika wametoa wito kwa serikali zote zilizokutana mwishoni mwa juma lililopita katika mkutano wa umoja wa mataifa kumweka mwanamke na msichana katika utashi wa maendeleo ya kitaifa na dunia mwaka 2015.
Mwaka huu malengo ya milenia yanafika ukingoni, na kuanzia septemba 25 malengo ya dunia kwa maendeleo endelevu ambayo yanalenga kuweka ajenda ya maendeleo kwa kizazi hiki ambapo tunaweza kushudia kizazi kikubwa chenye kuondoa umasikini uliokithiri. kama alivyowahi kusema Nelson Mandela.
Tayari kuna viashiria vya maendeleo, kwani mapema mwakwa huu Umoja wa Afrika AU wakuu wa nchi waliafiki kushughulika na ukweli kuwa umasikini unaathiri zaidi wanawake.
‘Nawaomba watanzania na waafrika kiujumla wasikilize wimbo huu kwani ukimyanyua msichana na mwanamke, utakuwa umenyanyua kila mtu, na nina hakika viongozi wamesikia wito wetu wa kunyanyua wasichana na wanawake kama ajenda muhimu. Ni wakati wa kutekeleza sasa’ anasema Diamond.
Kurudia wimbo wa Msichana Imara kwa kuwashirikisha wasanii wa kike na kiume si tu unaongeza nguvu ya ujumbe bali unaweka msisitizo wa kumwezesha mwanamke na kuonyesha ushirikiano baina ya wanamme na wanawake kuhakikisha wasichana na wanawake wanainuliwa.
Naye msanii D’Banj, anasema amepata heshima kubwa kuwa mshirika kwenye wimbo huu kwani ni muhimu kwangu kutumia muziki wangu kusaidia mabadiiko ya dunia na kuonyesha kuwa uwezeshaji wa wanawake ni suala la dunia nzima na ndio msingi wa kuondoa umaskini uliokithiri.
‘Wimbo huu ni zaidi ya wimbo au mwimbaji, na ni furaha kufahamu kuwa wakati wanamme ni sehemu ya tatizo, wamekuwa sehemu ya suluhisho’ anasema Bono, mwimbaji kiongozi wa U2.
Tanzania ni nchi muhimu kwa matokeo haya kwa kuwa na ushawishi mkubwa barani Afrika na baadhi ya mifano ya maendeleo kama Mpango mkakakati wa kitaifa kuhusu Maendeleo ya Jinsia (2005). Baadhi ya maeneo yanayohitaji kufanyiwa kazi:
- Usawa wa kijinsia umeendelea kuwepo kwa mujibu wa UNDP Maendeleo ya usawa wa kijinsia 2013 Tanzania inashikiria nafasi ya 159 kati ya nchi 187.
- Kuendelea kuwepo kwa maambukizi ya HIV/AIDS, ambayo kwa mujibu wa tume ya Taifa ya UKIMWI, maambukizi kwa wanawake ni (6.2%) kuliko wanamme (3.8%)
- Haki za Ardhi ni tatizo kubwa kwa wanawake wa Tanzania, wengi wanaathirika na masula hayo na kuathrili haki zao
![Processed with VSCOcam with x5 preset]()
You tube: https://www.youtube.com/watch?v=v-TGznFHHv0