NGULI wa muziki wa dansi, Nguza Vicking ‘Babu Seya’ na mwanaye Jonhson Nguza ‘Papii Kocha’ kwa mara ya kwanza tangu waachiwe huru Desemba 9 kwa msamaha wa Rais John Maguuli, leo Januari 5 wamekutana na Naibu Waziri wa Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo, Juliana Shonza pamoja na wanahabari ambapo wamepata fursa ya kueleza namna walivyojipanga kurudi kwenye tasnia ya muziki.
Akizungumza na wanahabari katika Studio za Wanene Entertainment zilizopo Mwenge, Coca-cola, Naibu Waziri Shonza amesema wao kama wizara kazi yao kubwa ni kuwasaidia wasanii na kuhakikisha wanafanikiwa kufikia malengo yao, hivyo wameamua kuwakutanisha na wadau wa muziki wakiwemo Wanene ili kufanmikisha zoezi la nguli hao kurudi kwenye game.
Twitter: @chokadj @DJChokaUpDates
Instagram: @ChokaDJ @DJChokaUpDates @djchokamusic
Facebook Fans Page: https://www.facebook.com/djchokamusic
Download DJChokaMusic Android Application Click HERE