Quantcast
Channel: News – eNCA Online TV
Viewing all articles
Browse latest Browse all 784

Unaambiwa hii ndio nchi ambayo haijafanya mitihani ya kidato cha nne ndani ya miaka 25

$
0
0

150616131710_mtihani_wa_kwanza_somalia_katika_miaka_25_624x351_bbc_nocredit

Zaidi ya wanafunzi elfu 70 walifanya mitihani ya kidato cha nne katika maeneo ya kusini na kati mwa Somalia, ikiwa ni mitihani ya kwanza ya kitaifa katika kipindi cha miaka 25.

Mitihani hiyo itaendelea kwa muda wa siku tano zijazo.

Katika mji mkuu wa Somalia Mogadishu, vituo 11 vilianzishwa kuwawezesha watahiniwa kufanya mitihani.

150616132047_mtihani_wa_kwanza_somalia_katika_miaka_25_624x351_bbc_nocredit

Elimu ni mojawapo ya sekta zilizoathirika vibaya na vita vya wenyewe kwa wenyewe vilivyoanza nchini Somalia mwaka wa 1991.

Tangu kusambaratika kwa serikali kuu nchini Somalia, mitaala mbali mbali imetumika katika shule na kufunzwa katika lugha tofauti tofauti.

Sasa wizara ya elimu inasema imechukuwa hatua za kuunganisha mitaala hiyo na kuhakikisha kuwa wanafunzi kote nchini wanafanya mtihani mmoja wa kitaifa.

Licha ya pingamizi kutoka kwa makundi mbali mbali yaliyoyounda mitala hiyo katika shule za kibinafsi nchini Somalia, serikali iliidhinisha kufanyika kwa mitihani huu.

Waziri wa elimu wa Somalia Khatra Bashir Ali ambaye alikuwa miongoni mwa maafisa waliosimamia mitihani hiyo, alisema nchi hiyo ina mengi ya kufanya katika ulimwengu wa sasa unaoegemea mfumo wa digitali.

Wengi wa wanafunzi waliofanya mitihani hiyo walikuwa na furaha.

Stori hii inaendelea hapo>>> BBC SWAHILI


Twitter: @chokadj @djchokatv

Instagram: @djchokatv @chokadj @djchokamusic

Facebook Fans Page: https://www.facebook.com/djchokamusic

Download DJChokaMusic Android Application Click HERE


Viewing all articles
Browse latest Browse all 784

Latest Images

Trending Articles



Latest Images