Umeshangaa? Sasa elewa ukweli Mpya huu kutoka kwa Hit Maker wa BADO Harmonize.
Amefunguka Kwa mara ya kwanza kupitia kipindi cha Funiko Base la Radio5 Wakati anatwangwa Maswali na DjHaazu ambapo kwenye swali la msingi kwamba ana msichana yeyote anayetoka naye kimapenzi au yupo single ndipo Harmonize akatirirka kwa majibu haya hapa chini:-
“Kwakweli bado lakini niko mbioni mbioni kumchukua mtoto mmoja wa Kiarusha Mtoto mmoja wa Chugga huko, hii taarifa naweka wazi kwanini sifiche kwanini nisiweke wazi naamini wengi wanamjua ni mtu maarufu sababu nataka kuwa na mtu maarufu mwenzangu umaarufu wetu tutautengeneza kutufanya tuje kuwa na familia bora ni mtu maarufu wengi wanamfahamu ila muda ukifika nitamtaja ni mtoto kutoka Chugga hapo”.
Aliposisitizwa Amtaje jina alijibu Sasa hawezi kumtaja ila tujue ni mtoto mzuri kutoka Arusha na ni mtu maarufu ila kwake ni wife Material .
SIKILIZA FULL INTERVIEW HAPA CHINI
Twitter: @chokadj @djchokatv
Instagram: @djchokatv @chokadj @djchokamusic
Facebook Fans Page: https://www.facebook.com/djchokamusic
Download DJChokaMusic Android Application Click HERE