Msanii anayeunda kundi la WEUSI anajulikana kwa jina la G NAKO muda mfupi uliopita amezungumza na DJ Choka kuhusu kuvuja kwa video yake mpya inayoitwa AROSTO akiwa amewashirikisha wasanii wenzake Nikki wa II na Chin Bees. G Nako anasema kuwa Dir wa video hiyo ambaye anaitwa Nisher alipost link ya video hiyo kwa bahati mbaya na watu wakainyonya na kuweka katika channel zao za YouTube. Namnukuu
“Video official bado haijatoka kwasababu kuna vitu bado vinatakiwa kueditiwa katika video ya Arosto ili itoke official video, ila Ijumaa hii naachia Audio ya Arosto official kwenye Radio”
Twitter: @chokadj @djchokatv
Instagram: @djchokatv @chokadj @djchokamusic
Facebook Fans Page: https://www.facebook.com/djchokamusic
Download DJChokaMusic Android Application Click HERE