Quantcast
Channel: News – eNCA Online TV
Viewing all articles
Browse latest Browse all 784

MSANII WA NIGERIA – RAVE AACHIA WIMBO NA VIDEO MPYA YA ‘TONIGHT’

$
0
0

aaa

Cadilly Entertainment wanamleta kwako msanii wa Nigeria,  Wilfred Utere, anayejulikana zaidi kwa mashabiki wake kwa jina la Rave akiwa na kazi yake mpya, iitwayo TONIGHT.  Mtumbuizaji huyo mwenye vipaji vingi vikiwemo uchezaji dansi na anajulikana zaidi kwa kushinda shindano la kucheza muziki la Nigeria ‘National ‘Maltina Dance All’ msimu wa nane (2014).

Video ya TONIGHT ilifanyika huko Port Harcourt nchini Nigeria na kuongozwa na muongozaji mwenye kipaji, Eddie iZcs wa EMPRESSIONISTO.

Kwenye TONIGHT,  Rave anaonesha mitindo ya kuvutia ya uchezaji unaofanya mashabiki waone upande wake mwingine: muziki wa kipekee utakaokushawishi kuinuka na kucheza.  Rave amepania kuleta uchezaji wake wa nguvu na muziki wake Afrika Mashariki.  Akitarajia kufanya ziara Afrika Mashariki,  Rave anasema, “ Ndoto yangu siku zote imekuwa kuwafikia na kuwahamasisha vijana, hivyo kitendo cha kuweza kuwafikia vijana wa Afrika Mashariki, kimevuka matarajio yangu ya awali. Ninachoweza kusema kwa sasa ni Asante Sana! Naahidi kuja na muziki mzuri, mpya na wa tofauti. Kupitia muziki wangu nataka kuonesha upande mwingine wa Afrika kuwa ni sawa kutoka nje ya boksi na kufanya kitu tofauti.”

ITAZAME  ‘TONIGHT’

YouTube: youtu.be/4sQnNASMVE0

Video ya kwenye simu: goo.gl/ffwZhp

Hulkshare: bit.ly/TonightRAVE


Twitter: @chokadj @djchokatv

Instagram: @djchokatv @chokadj @djchokamusic

Facebook Fans Page: https://www.facebook.com/djchokamusic

Download DJChokaMusic Android Application Click HERE


Viewing all articles
Browse latest Browse all 784

Latest Images

Trending Articles



Latest Images